Wafanyakazi wa Twitter wenye ulemavu wajiuzulu baada ya kushindwa masharti

0
37

Baada ya mmiliki wa Twitter, Elon Musk kutangaza kuongeza saa za kazi kwa wafanyakazi wake, wafanyakazi wenye ulemavu wameamua kujiuzulu baada ya kuhisi hawawezi kufikia kiwango cha utendaji  kutokana na ulemavu wao.

Kesi hiyo iliyowasilishwa kwa niaba ya Dmitry Borodaenko, Mhandisi aliyeachishwa kazi mapema mwezi huu, aliishutumu Twitter kwa kuvunja sheria za ubaguzi na kudai yeye ni mwathirika wa saratani ambaye alifukuzwa kazi baada ya kumwambia meneja wake angependa kufanyia kazi nyumbani kwa sababu alikuwa kwenye hatari zaidi ya  UVIKO-19.

“Wafanyakazi wengi walemavu ambao wamefanya kazi zao kwa ufanisi na ambao wangeendelea kufanya kazi zao kwa ufanisi wamehisi kwamba, kwa sababu ya ulemavu wao hawataweza kufikia kiwango hiki kipya cha utendaji na tija. Kwa hivyo, wafanyakazi wengi walemavu wamehisi kulazimishwa kujiuzulu,” ilisema taarifa ya kesi hiyo.

Kesi hiyo ilidai, wafanyakazi kama Borodaenko bado walikuwa na uwezo wa kufanya kazi zao kwa ufanisi, lakini kauli ya mwisho ya Musk kuhusu ongezeko la saa za ziada na kuondoa kufanyia kazi nyumbani, hairuhusu wafanyakazi ambao wanahitaji muda wa kutosha kwa ulemavu wao.

“Tabia ya Elon Musk tangu achukue Twitter wiki kadhaa zilizopita imekuwa ya kustaajabisha. Sijawahi kuona kitu kama hiki katika takriban robo karne yangu” amesema wakili wa Borodaenko katika taarifa yake.

 

 

Send this to a friend