Wafanyakazi wa uwanja wa ndege warejesha begi la mtalii lililokuwa na TZS milioni 44

0
24

Wafanyakazi wawili wa uwanja wa ndege wa Kenya na afisa wa Polisi wamejizolea sifa baada ya kurudisha begi lililokuwa limebeba takriban $19,000 (sawa na TZS milioni 44.3) na vitu vingine vya thamani kwa mtalii kutoka nchini Uingereza.

Mtalii huyo alikuwa katika kundi ambalo lilikuwa limerejea kutoka safarini katika mbuga ya wanyama ya Maasai Mara na ndipo alipopoteza begi lake katika uwanja wa ndege wa Wilson katika mji mkuu, Nairobi.

Wafanyakazi wa uwanja huo wa ndege na afisa Polisi mwanamke walilipata begi hilo na kulikagua kabla ya kuwasiliana na mmiliki.

Aina 5 za mipaka unazostahili kuwa nazo katika maisha

“Pesa zote za jumla ya dola 19,000 na baadhi ya maelfu ya shilingi za Kenya zote zilikuwa ziko sawa. Kadi zangu zote zilipatikana. Vitu vingine vyote vya thamani vilivyojumuisha mavazi niliyopewa na marehemu bibi yangu pia vilipatikana Ilikuwa ni kama ndoto ya mchana,” mtalii Benson Nickolson ameandika katika barua pepe ya shukrani kwa polisi wa Kenya.

Msimamizi wa usalama wa uwanja huo wa ndege, Joseph Kabangi ameiambia kituo cha habari cha Citizen ya nchini Kenya kuwa “uadilifu ndio thamani kuu” miongoni mwa wafanyikazi katika uwanja huo.

Send this to a friend