Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc watoa msaada wa vifaa mbalimbali vya shule vyenye thamani ya zaidi ya TSh. Milioni 21 kwa kituo cha kulelea Watoto yatima Kiwalani
Mkurugenzi wa TEHAMA wa Vodacom Tanzania, Athumani Mlinga (wa tatu kulia) akimtamza mwanafunzi wa shule ya kituo cha kulelea Watoto yatima cha Kiwalani, Janeth Lwanga (wa kwanza kushoto) akisoma mojawapo ya kitabu vilivyokabidhiwa kama msaada wa vifaa mbalimbali vya shule kama vile madawati, meza, viti, vitanda, magodoro, na kompyuta vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 21 kwa niaba ya wafanyakazi wa kampuni hiyo mwishoni mwa wiki. Wakifuatilia tukio hilo ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kiwalani, Bw. Leornard Kingu Msusu (wa kwanza kulia), Afisa Mtendaji wa Kata ya Kiwalani, Bi. Lucresia Francis Shayo (wa pili kulia) pamoja na Mwalimu wa kituoni hapo, Bi. Yustina Myovera (nyuma ya mwanafunzi).
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Bi Vivienne Penessis (katikati), na Mkurugenzi wa TEHAMA, Bw. Athumani Mlinga (wa pili kulia) kutoka Vodacom Tanzania Plc, wakikabidhi baadhi ya msaada wa vitabu pamoja na vifaa vinginevyo vya shule kwa Mwasisi na Mwanzilishi wa kituo cha kulelea Watoto yatima cha Kiwalani, Mchungaji Elias Mwakalukwa (wa kwanza kushoto) na mwanafunzi wa shule ya kituoni hapo, Cecilia Teotimo (wa pili kushoto) wakati Afisa Mtendaji wa Kata ya Kiwalani, Bi. Lucresia Francis Shayo (wa kwanza kulia) akishuhudia tukio hilo.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania walikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya shule kama vile vitabu, madawati, meza, viti, vitanda, magodoro, na kompyuta vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 21 ikiwa ni jitihada za kuisadia jamii mwishoni mwa wiki.