Wafikishwa mahakamani kwa kuwahadaa wanaume kimapenzi na kuwaibia

0
61

Washukiwa watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Sheria ya Embu nchini Kenya kwa makosa ya kuwahadaa wanaume na kuwaibia pesa.

Washtakiwa hao ni Virginia Njagi, Erick Bundi na Kelvin Kathenya ambao wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkuu Robert Mundia na kusomewa mashtaka matatu yaliyofanywa katika wakati tofauti.

Wanafamilia saba wakamatwa kwa kumchapa viboko ndugu aliyehudhuria maombi

Watu hao wakiwemo wanaume wawili na mwanamke mmoja, imeelezwa kuwa hupanga njama ambapo mwanamke huyo hukutana na mwanaume katika chumba cha kukodi, na wanaume wengine wawili huvamia na kumshtaki mlengwa kwa kushiriki ngono na mke wa mmoja wao kisha kuomba malipo.

Wakisomewa mashtaka yao, mahakama imeeleza kuwa mnamo Aprili 10, mwaka huu huko Embu Magharibi, kwa pamoja wakiwa wamebeba fimbo walivamia katika nyumba ya kulala wageni, na kumpora mwanaume aliyekuwa na miadi na mwanamke huyo kiasi cha Ksh.11,100 [TZS 217,033] mara baada ya kumfanyia vurugu.

Send this to a friend