Wafuasi 40 wa Zumaridi waliokataa dhamana, leo wakubali na kuachiwa

0
12

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza imewaachia kwa dhamana washtakiwa 40 kati ya 85 wa kesi namba 12/2022 inayomkabili Diana Bundala maarufu kama ‘Mfalme Zumaridi’ na wafuasi wake.

Mfalme Zumaridi na wafuasi wake walifikishwa katika mahakama hiyo Machi 3, 2022 na kusomewa mashtaka matatu ambayo ni kuzuia maofisa wa Serikali kutekeleza majukumu yao, kufanya mkusanyiko usiyo na kibali na shtaka la usafirishaji haramu wa binadamu lililokuwa likimkabili Mfalme Zumaridi peke yake.

Washtakiwa hao baada ya kusomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Monica Ndyekubora kisha kupewa nafasi ya dhamana walikataa kupewa dhamana kwa madai kwamba wako tayari kuendelea kusota rumande na kiongozi wao.

Akizungumza baada ya kutolewa kwa dhamana hiyo leo Jumatano Machi 9, 2022, Wakili wa washtakiwa hao, Erick Mutta amesema dhamana hiyo imetolewa baada ya mshtakiwa namba moja wa shauri hilo (Mfalme Zumaridi) kuiomba mahakama hiyo kuwaachia kwa dhamana washtakiwa wanaoweza kudhaminika katika kesi hiyo.

Send this to a friend