Wafuasi wa Zumaridi ‘wamsaliti’ gerezani

0
48

Wafuasi wa mshtakiwa Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi, anayekabiliwa na kesi ya kusafirisha binadamu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Mwanza wamebaki watano kati ya 91 waliokataa dhamana tangu walipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Machi 3 mwaka huu.

Watuhumiwa hao wanaoshtakiwa kwa kosa la kufanya kusanyiko lisilo halali na wanane kati yao wakituhumiwa kufanya shambulio la kudhuru mwili, walikataa dhamana siku ya kwanza mahakamani na kusisitiza kukaa na mtuhumiwa Zumaridi gerezani.

Aidha, wafuasi hao wameendelea kubadili misimamo yao mbapo Machi 31 idadi ya wafuasi ilikuwa saba, mpaka kufikia jana wafuasi wengine wawili walikukubali dhamana na kuwaacha wafuasi watano ambao wameendelea kushikilia msimamo wa kutokubali kudhaminiwa kwa madai kuwa wapo tayari kufa na mfalme wao.

Wakili wa washtakiwa hao, Eric Mutta amesema washtakiwa hao watano bado wameendelea na msimamo wao wa kutokubali dhamana, yeye kama wakili wao hawezi kuwalazimisha wakubali isipokuwa wanaendelea kuwashauri na siku wakikubali watadhaminiwa.

Send this to a friend