Wagoma kuchukua mwili wakidai kijana wao alikuwa na ugomvi na uongozi wa shule

0
31

Ndugu wa mwanafunzi, Julius Nchagwa aliyekuwa akisoma Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Mogabiri iliyopo wilayani Tarime mkoani Mara, ambaye alifariki baada ya kuanguka katika uwanja wa shule hiyo muda mfupi baada ya kutoka kwenye chumba cha mtihani, wamegoma kuuchukua mwili wakidai kijana wao alikuwa na ugomvi na uongozi wa shule.

Akizungumza mzazi wa mwanafunzi huyo, Daniel Marwa amesema hawako tayari kuuchukua mwili huo huku wakishinikiza uchunguzi ufanyike kwakuwa kuna utata juu ya kifo cha kijana wao akieleza kuwa miezi kadhaa kijana wao alikuwa na ugomvi na uongozi wa shule nakupelekea kusimamishwa masomo yake.

“Wanafamilia tumeshauriana kwanza tusichukue mwili wa marehemu hadi taratibu zote za uchunguzi zitakapofanyika kwa kuwa kifo cha kijana wetu kina utata kutokana na kuwepo kwa ugomvi baina yake na uongozi wa shule hapo awali,” amesema.

Aidha, kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mwanafunzi huyo alikuwa akitetemeka na kupelekea kuanguka kwenye uwanja wa mpira na kupoteza fahamu ambapo inadaiwa kuwa alipoteza maisha kabla hajapatiwa matibabu.

Send this to a friend