Wagombea wa CCM watakiwa kubadili maudhui ya kampeni zao

0
30

Siku mbili baada ya kuzindua awamu ya sita ya kampeni zake, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally amewataka wagombea wa chama hicho katika ngazi zote nchini kubadilisha maudhui ya kampeni zao kwenye majukwaa.

Akizungumza akiwa mkoani Mwanza Dkt. Bashiru amesema kuanzia sasa maudhui ya wagombea wa CCM yawe ya kuwaandaa wapiga kura kujitokeza kwa wingi kuchagua wagombea udiwani, ubunge na Rais wa chama hicho.

Oktoba 14 mwaka huu chama hicho kilitangaza kuzindua awamu ya sita ya kampeni zake na kueleza kuwa awamu hii ya lala salama itajikita katika kutoa elimu ya uchaguzi kwa wapigakura na mawakala ili kuhakikisha kinajiongezea nafasi ya ushindi.

Send this to a friend