Wagonjwa wa Corona Tanzania wafikia 12

0
33

Rais Dkt Magufuli ametangaza kuwa idadi ya watu wenye maambukizi ya virusi vya Corona nchini Tanzania imeongezeka na kufikia 12 kutoa sita wa awali.

Rais ameeleza hilo katika tamko lake kwa umma kuhusu ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na na virusi hivyo alilolitoa leo Machi 22, 2020, Ikulu Dodoma.

“Mpaka sasa, nchi yetu imebaini wagonjwa (12) ambao wamethibitika kuambukizwa ugonjwa huu wa korona. Kati yao wanne (4) ni raia wa nje na wanane (8) ni raia wa Tanzania,” ameeleza Rais Magufuli.

Aidha, ameeleza kuwa wagonjwa wote, isipokuwa mmoja, ametoka kwenye nchi zilizokuwa zimebainika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo, na pia wagonjwa hao wanaendelea vizuri.

Send this to a friend