Wahamiaji 14 wamefariki baada ya boti kushika moto

0
39

Takribani wahamiaji 14 wamefariki baada ya boti waliokuwa wakisafiria kuungua moto Kusini mwa nchi ya Senegal.

Mamlaka nchini humo zimesema zimefanikiwa kupata miili 14 baada ya tukio hilo la moto lililotokea Jumatatu, pamoja na msako wa kuwatafuta ambao hawajapatikana ukiendelea.

Aidha Muuguzi mkuu, Bourama Faboure amesema watu 21 wamejeruhiwa wakiwemo wanne waliopata majeraha ya moto daraja la pili.

Wenye ulemavu Tanzania wanavyosafirishwa na kutumikishwa Kenya

Meya wa eneo hilo, David Diatta amesema walionusurika katika janga hilo wamedai moto huo uliwashwa na mtu aliyekuwa akivuta sigara karibu na eneo ambapo mafuta yaliwekwa.

Hata hivyo, idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka kutokana na boti hiyo kuwa na wahamiaji wengi ambao wametambuliwa kuwa ni raia wa Guinea, Nigeria, Gambia na Senegal.

Send this to a friend