Wahamiaji 40 wafariki baada ya boti kuwaka moto

0
40

Wahamiaji takriban 40 wamefariki baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kutoka Cap-Haitien kwenda Visiwa vya Turks na Caicos kuungua moto katika Pwani ya Kaskazini mwa Haiti.

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema Chanzo cha moto huo bado hakijabainika, lakini afisa mmoja wa eneo hilo aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa watu waliokuwa kwenye boti hiyo walikuwa wakiwasha mishumaa katika ibada ya kuombea safari hiyo, na kusababisha matanki yaliyojaa petroli kuwaka moto.

Aidha, IOM imebainisha kuwa wahamiaji wengine 41 wameokolewa na walinzi wa Pwani ya Haiti, na sasa majeruhi wote wanapatiwa matibabu.

Maelfu ya watu huikimbia Haiti kila mwaka kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo changamoto za umaskini, uasi, sheria na ghasia za magenge nchini mwao.

Send this to a friend