Wahitimu 118 hatarini kufutiwa PhD zao

0
34

Wahitimu 118 wa Shahada za Uzamivu (PhD) mwaka 2019 kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jomo Kenyatta nchini Kenya wapo hatarini kufutiwa shahada zao kufuatia kukiukwa kwa taratibu katika kuhitimu kwao.

Tume ya Vyuo Vikuu nchini Kenya (CUE) imetoa miezi mitatu kwa Seneti ya Chuo kupitia shahada hizo zilizotolewa katika mahafali ya 33.

Mbali na hilo, chuo hicho kimetakiwa kusitisha kutoka PhD kwenye matawi yake kutokana na kutokuwa na uwezo, ambapo imetolewa mfano wa tawi la Mombasa lililotoa PhD 23 kwa miaka mitatu illiyopita, lakini tawi hilo halina profesa hata mmoja.

Chuo hicho kimetakiwa tuo majibu ya maswali yaliyoibuliwa na tume hiyo, vinginevyo shahada hizo zilizotolewa zitafutwa mara moja. Pia tume hiyo itapitia PhD zote zilizotolewa katika mahafali tatu zilizopita.

Jumla ya PhD 327 na Shahada za Umahiri (2,101) zimetolewa katika mahafali ya 31, 32 na 33 yaliyofanyika Juni 2018, Novemba 2018 na Juni 2019.

Miongoni mwa mambo yaliyoelezwa kukiukwa na kutokuwepo kwa usimamizi wa karibu kwa wanafunzi wa PhD kutoka kwa wakufunzi wao na pia kutofuatwa kwa taratibu katika uundaji wa bodi ya wasimamizi, usimamizi wa semina za wanafunzi pamoja na upangaji wa wasimamizi watakaaowaongoza wanafunzi kuandaa machapisho yao (thesis).

Bodi ya wasimamizi iliyoundwa na chuo kupitia machapisho ya wanafunzi ilikuwa na watu wanne, wakati kanuni za vyo zinataka bodi hiyo kuwa na si chini ya watu 6 waliokidhi vigezo.

Pia hakukuwa na uthibitisho wa kukutana kati ya msimamizi na mwanafunzi wakati wa kuandaa machapisho, kwani hakuna rekodi inayoonesha kuwa walikutana.

Wanafunzi wake waliweka machapisho yao katika jarida la AJPO ambalo wakufunzi wengi wa Kitivo cha Maendeleo ya Rasilimali Watu (CoHRED) wana maslahi nalo.

Baadhi ya wanafunzi walimaliza kuandaa thesis zao ndani ya muda mfupi (miezi 12) jambo ambalo linatia mashaka kuhusu ubora wa machapisho hayo.

Send this to a friend