
Wanandoa Mitchell na Jennifer wamesema abiria alifariki ndani ya ndege ya Qatar Airways iliyokuwa ikitoka Melbourne kwenda Doha, na kwakuwa alikuwa na mwili mkubwa kuhamishwa, wahudumu walilazimika kumlaza kwenye kiti karibu na Mitchell kwa saa nne za mwisho wa safari akiwa amefunikwa kwa blanketi.
Wanandoa hao wamelalamika kuwa tukio hilo lilikuwa la kushtua, hasa kwa sababu hakuhamishwa licha ya kuwepo viti vilivyo wazi.
Wakati huo, Bi. Jennifer amesema alialikwa na abiria mwingine kuketi naye upande wa pili wa njia, lakini Ring amesema wafanyakazi wa ndege hawakumpa nafasi nyingine licha ya kuwepo viti vilivyo wazi karibu.
Qatar Airways imejibu kuwa wahudumu walifuata taratibu sahihi na walijaribu kuwahamisha abiria waliokuwa karibu, na mmoja wao kukaa na mwili wa marehemu hadi walipotua Doha.
Shirika hilo limesema lilishaomba radhi katika taarifa ya awali kwa usumbufu au msongo wa mawazo ambao tukio hilo huenda limesababisha.