Wajumbe wa bodi anayoingoza Jenerali Mabeyo wateuliwa

0
19

Kufuatia Rais Samia Suluhu Hassan kumteua Jenerali (Mst) Venance Mabeyo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) Juni 30, 2022, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana amewateua wajumbe.

Aliwateua ni;

Benson Obdiel Kibonde, Mhifadhi Wanyamapori Mkuu (Mst) Pori la Akiba Selous.

Bakari Nampenya Kalembo – Mshauri wa Masuala ya Fedha.

Agnes Kisaka Meena, Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Prof. Esther William Dungumaro, Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu, Mkwawa (MUCE).

Prof. Herrieth Godwin Mtae, Mtaalamu wa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Prof. Henry Chalu, Profesa Mshiriki, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Simon Vedastus Ntobbi, Afisa Tawala Mkuu Daraja la I, Ofisi ya Rais – UTUMISHI.

Uteuzi huo ni wa miaka mitatu kuanzia Julai 20, 2022 hadi 19 Julai, 2025.