Wakala wa mabasi: Tungeendelea kuwasubiri Latra tungeumia

0
52

Wakati Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) ikitangaza mabadiliko ya nauli za mabasi na daladala yatakayoanza Mei 14 mwaka huu, baadhi ya wakala wa mabasi wameeleza kuwa tayari wameshaanza kutumia viwango hivyo mara baada ya bei ya mafuta kupanda.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi, Tito Juma wakala wa basi linalofanya safari zake Dar es salaam kwenda Dodoma katika stendi ya Magufuli amesema kuwa, ni takribani wiki ya pili sasa wanatoza shilingi 26,000 badala ya 24,000.

“Siku mafuta yalipopanda na sisi tulipandisha bei siku ile ile, tuliwakilisha maombi kwa Latra jana [juzi] ndiyo wamejibu na kutoa taarifa hiyo, kwa maana tungewasubiri tungeendelea kuumia, tumejiongeza. Utasubiri siku 14 wakati huo unamwambia nini mmiliki, yeye anataka faida,” amesema.

Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Ngewe amewaonya wote walioenda kinyume na agizo hilo na alisema kuwa sheria inawataka kabla ya kutoza nauli mpya wampe taarifa abiria ndani ya siku 14 na wao watachapisha katika gazeti la Serikali.

Send this to a friend