Wakamatwa kwa kumuua mwanamke kisa wivu wa mapenzi

0
42

Jeshi la Polisi mkoani Kagera limewakamata watuhumiwa wawili waliokuwa wakitafutwa kwa tuhuma za mauaji ya Editha Anderson (32) mkazi wa Mtaa wa Kilimahewa, Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera chanzo kukuwa ni wivu wa mapenzi.

Watuhumiwa hao ni Answari Mutalemwa (25), na Kenedi Muganyizi (25) wote wakiwa wakulima na wakazi wa Mtaa wa Kashenye kata ya Kashai, Tarafa ya Rwamishenye, Manispaa ya Bukoba.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema watuhumiwa walitekeleza mauaji hayo Desemba 12, 2024 huko Mtaa wa Kalimahewa ambapo inaelezwa kuwa mtuhumiwa Mutalemwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Editha na wakiw katika mahusiano alibaini kuwa mpenzi wake alikuwa na mahusiano na mwanaume mwingine kitendo ambacho kilimchukiza.

Baada ya kubaini hilo, imeelezwa kuwa alimshirikisha mwenzake, kisha waliamua kumuua Editha na kuchukua simu yake ya mkononi kisha Muganyizi akaificha simu hiyo ili isipatikane tena.

Send this to a friend