Wakamatwa mkoani Pwani na vifaa vya kutengeneza fedha bandia

0
68

Watu wawili raia wa Afrika Magharibi wamekamatwa na Maofisa Uhamiaji Mkoa wa Pwani wakiwa na karatasi za kuchapisha pesa bandia, kemikali na kasiki (safe) la kutunzia fedha eneo la Mapinga, Bagamoyo mkoani humo .

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amewataja watu hao waliokamatwa kuwa ni Livingstone Ese Onayomake (raia wa Nigeria) na Bertrand Noubissie (raia wa Cameroon).

Kunenge amesema Februari 9, 2023 walipokea taarifa za kiintelijensia kuhusu watu wanaotiliwa mashaka, na siku iliyofuata ulifanyika upekuzi na kuwakamata raia hao ambao wamekutwa pia na hati za kusafiria 34 za nchi za Nigeria na Ghana.

Amesema wakati wa upekuzi mtuhumiwa Onayomake alikutwa na paspoti 34 ambazo si zake, kati yake 32 ni za Nigeria na mbili za Ghana, na alipofanyiwa mahojiano mnaigeria huyo alidai alichukua paspoti hizo kwa lengo la kuwatafutia wahusika viza ya Uturuki.

Aina16 za vitabu zilizopigwa marufuku kutumika shuleni nchini

“Jambo la kusikitisha raia hao walikutwa wakihifadhiwa na Mtanzania, na mbaya zaidi mmoja alishaanza kujihusisha na utengenezaji wa fedha bandia maana alikutwa karatasi zilizoandaliwa kwa ajili ya kuchapisha noti bandia, kemikali pamoja na kasiki (safe) la kutunzia fedha,” amesema Kunenge.

Naye Afisa uhamiaji Mkoani Pwani, Omary Hassan amesema baada ya kupata taarifa walienda kufanya upekuzi kwenye makazi waliokuwa wakiishi na kwamba wahamiaji hao walikuwa wakiishi nyumbani kwa New Era Nyirembe ambaye alikuwa mke wa mtuhumiwa Noubissie ambaye kwa sasa ni marehemu.

Send this to a friend