Wakamatwa wakidaiwa kuuza mishikaki ya nyama ya Mbwa Msamvu

0
21

Waswali husema, ukimchungaza sana bata hutamla, lakini wakati mwingine ni heri uchungeze ili ujue unachokula ni nini.

Watu watatu wamekamatwa baada ya kukutwa wakimchuna mbwa ngozi kwa ajili ya kuandaa mishikaki katika Kituo cha Mabasi Msamvu mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa gazeti l The Citizen watatu hao wamekamatwa mchana kweupe baada ya baadhi ya watu kuwa na mshaka juu ya mnyama waliyekuwa wakimchuna ngozi.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliohojiwa na gazeti hilo wamesema mara tu walipoona kichwa cha mnyama huyo ndipo walitambua kuwa alikuwa mbwa jambo ambalo liliwashitua sana.

Kukamatwa kwao kumewaacha wananchi na mshangao hasa madereva bodaboda ambao wamekiri kuwa wamekuwa wateja wazuri wa kula mishikika ya wafanyabiashara hao.

“Nimekuwa nikinunua mishikaki kutoka kwao, lakini hatukuwa tunajua kwamba wanatulisha nyama ya mbwa muda wote huo, jambo ambalo ni kinyume na tamaduni zetu kwa sababu mbwa kwetu ni rafiki anayetuweka salama na si vinginevyo,” amesema Samson Jonas.

Send this to a friend