Wakamatwa wakijaribu kutapeli kwa kuuza madini hospitalini

0
46

Watu wawili wanaoshukiwa kuwa ni matapeli wamekamatwa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road walipokuwa wakijaribu kumtapeli moja ya kati ya ndugu wa wagonjwa hospitalini hapo.

Akisimulia kuhusu kisa hicho, mwanamke huyo ambaye jina lake limehifadhiwa amesema watu hao ambao majina yao ni Bakari Rajabu na Twaha walijifanya kuwa ni wachimbaji wadogo wa madini na kutaka kuoneshwa mahali linapopatikana duka la kuuzia madini hayo ya dhahabu.

Hata hivyo, baada ya kushtukiwa njama zao walitaka kutoroka ndipo alipotoa taarifa kwa askari wa usalama wa taasisi hiyo na watu hao kukamatwa.

Kwa upande wa watuhumiwa wamekiri kufanya tukio hilo wakijitetea kuwa pilika pilika za maisha ndizo zimefanya kujaribu kufanya utapeli huo.

Kupitia taarifa iliyotolewa na wizara ya afya imewatahadharisha wananchi pindi wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kuhakikisha wanapitia na kufata taratibu zote kwenye njia stahiki na kujiepusha na mazungumzo na watu wasiowajua.

Send this to a friend