Wakamatwa wakiuza sehemu za siri za mwanaume

0
47

Mamlaka ya Msumbiji inawashikilia wanaume wawili kwa madai ya kujaribu kuuza sehemu za siri za mwanaume zilizo na majeraha.

Viungo hivyo vilivyokuwa vikiuzwa kwa gharama sawa na TZS milioni 97.5 zimedaiwa kutolewa katika mwili wa mwanaume mmoja aliyeuawa katika eneo la Milange jimbo la Zambézia nchini Malawi.

Awali washukiwa hao wa ulanguzi wenye umri wa miaka 29 na 32 inasemekana waliwasiliana na mfanyabiashara wa eneo hilo, António Chicopa na kumpendekeza kununua viungo hivyo.

Hata hivyo mfanyabiashara huyo aliwasiliana na mamlaka za eneo hilo, na baadaye walifika kwa kushtukiza na kufanikiwa kuwakamata.

Kamanda Polisi wa wilaya ya Milange, Alice Evaristo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema washukiwa hao wawili wako chini ya ulinzi wa polisi wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Send this to a friend