Wakandarasi waliojenga majengo yaliyoporomoka Uturuki wakamatwa

0
43

Maafisa nchini Uturuki wametoa vibali 113 vya kukamatwa kwa watu waliohusika na ujenzi wa majengo yaliyoporomoka katika tetemeko la ardhi liliotokea siku ya Jumatatu

Tayari watu wasiopungua 12, wakiwemo wakandarasi wa ujenzi wamekamatwa na polisi nchini humo.

Inaelezwa kuwa kwa miaka mingi, wataalam walionya kuwa majengo mengi mapya nchini Uturuki hayakuwa salama kutokana na ufisadi uliokithiri na sera za serikali kwa mujibu wa BBC.

Sera hizo ziliruhusu kinachojulikana kama msamaha kwa wakandarasi waliokiuka kanuni za ujenzi, ili kuhimiza ukuaji wa ujenzi, ikiwa ni pamoja na katika maeneo yanayokumbwa na tetemeko la ardhi.

Idadi ya watu waliothibitishwa kufariki mpaka sasa imefikia zaidi ya watu 28,000.

Send this to a friend