Wakazi 30,000 wa Dar na Mwanza wanaugua Saratani

0
39

Takribani asilimia 3.75 ya watu waliopimwa saratani chini ya Mradi Mtambuka wa Saratani Tanzania (TCCP) wamegundulika kuwa na ugonjwa huo, jambo ambalo limeonyesha haja ya kuongeza uelewa kwa Watanzania juu ya kupima afya zao.

Meneja mradi wa TCCP, Dkt. Harrison Chuwa amesema jumla ya watu 800,000, wakazi wa Dar es Salaam na Mwanza walipimwa wakati wa zoezi lililofanyika hivi karibuni ambapo kati ya idadi hiyo, 30,000 waligundulika kuwa na aina mbalimbali za saratani.

Zaidi ya asilimia 70 ya waliothibitishwa kuwa na saratani walikuwa katika hatua za juu za ugonjwa huo huku wanawake wengi wakigundulika kuwa na saratani ya shingo ya kizazi na matiti, wakati wanaume wakionekana kuwa na saratani ya tezi dume na utumbo mpana.

Kuchelewa kupima mara nyingi hutokea kutokana na ukosefu wa ufahamu au uelewa wa umuhimu wa kuchunguza afya mara kwa mara. Elimu sahihi inahitajika ili kuelimisha jamii juu ya dalili za awali za saratani na umuhimu wa kufanya vipimo vya mara kwa mara.

Send this to a friend