Wakazi wa Dar wapewa wiki 3 wawe wamepaka rangi majengo yao

0
111

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam amewatangazia wakazi wote wa jiji hilo, hususani maeneo ya Kariakoo, Mchikichini, Jangwani, Kivukoni, Kisutu, Gerezani, Mchafukoge, Upanga Mashariki na Upanga Magharibi kupaka rangi majengo yao.

Amehimiza zoezi hilo likamilike ifikapo Septemba 30, 2025 ikiwa ni mpango wa kuunga mkono juhudi zinazofanywa katika kuboresha mandhari ya Jiji la Dar es Salaam.

Aidha, taarifa hiyo iliyotolewa kwa umma imesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote ambaye hatatekeleza ndani ya muda uliopangwa.

Send this to a friend