Wakazi wa Dar watakiwa kuepuka matumizi ya maji yasiyo ya lazima

0
10

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amewataka wakazi wa Dar es salaam na Pwani kuhakikisha wanatumia maji kwa uangalifu na kujiepusha na matumizi yasiyo ya lazima.

Amesema Wizara ya Maji inaendelea na zoezi maalumu la kuhakikisha uchepushaji wa maji pamoja na shughuli mbalimbali za kibinadamu ambazo zinaathiri upatikanaji wa maji kwa wananchi zinakomeshwa.

“Niwahakikishie wananchi wa Jiji la Dar es saalam na wale wa mkoa wa Pwani. Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Dar es Salaam (DAWASA) tunaendelea na zoezi la kuzuia uchepushwaji wa maji katika vyanzo vyetu vya maji, pia  kuzuia shughuli za kibinadamu katika  kuhakikisha maji hayo yanaingia katika mzunguko wa huduma kwa wananchi kwa kusukumwa katika mitambo yetu ya Ruvu. Niwaombe sana, hakikisheni mnatunza maji. Matumizi ya maji yasiyokuwa ya lazima tuepukane nayo,” amesema Waziri Aweso

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema shughuli za utekelezaji wa mradi wa maji Kigamboni unakwenda vizuri.

Kukamilika kwa mradi wa maji Kigamboni kutawezesha upatikanaji wa lita za maji milioni 57 kwa siku. Mahitaji ya maji kwa mji wa Kigamboni kwa sasa ni lita Milioni 24 kwa siku

Send this to a friend