Meya wa kijiji cha Belcastro, Antonio Torchia, amewataka wakazi wa kijiji hicho cha kaskazini mwa Italia kuepuka kupata magonjwa yanayohitaji msaada wa dharura kutokana na upungufu mkubwa wa huduma za matibabu.
Amri hiyo, ambayo imetajwa kama ni “mzaha”, imeibua mjadala mkubwa nchini Italia huku ikilenga kuonyesha changamoto kubwa zinazoukumba kijiji cha Belcastro, ambacho kiko mbali na huduma za afya.
Katika amri hiyo, Torchia amewataka wakazi wa Belcastro kuepuka kushiriki katika tabia yoyote inayoweza kuleta magonjwa au ajali zinazohitaji huduma za dharura, akibainisha kuwa wanapaswa kuepuka ajali za nyumbani na pia kuepuka kutoka nje mara kwa mara, kusafiri, au kufanya michezo.
Belcastro, kijiji kidogo chenye wakazi 1,300, kinakumbwa na ukosefu wa huduma bora za afya, ambapo Meya huyo amekuwa akihamasisha viongozi wa kisiasa na mamlaka za mkoa kuhusu hali hiyo.
Torchia amesema kuwa Idara ya Dharura na Ajali iliyo karibu, iko zaidi ya kilomita 45 (maili 28) kutoka kijijini, na barabara inayounganisha kijiji hicho na idara hiyo ina kikomo cha kasi cha kilomita 30 kwa saa.