Wakazi wa Ngorongoro wadai kutishiwa wasizungumze na vyombo vya habari

0
58

Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro mkoani Arusha, Edward Maura amesema wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakipata vitisho mbalimbali ili wasizungumze na vyombo vya habari kuhusu changamoto wanazopitia.

Amesema vitisho hivyo vinakuja baada ya kueleza shida wanazopitia ikiwemo ukosefu wa huduma bora za afya, mazingira magumu ya elimu kwa watoto wao na hata kuzorota kwa huduma za kimaendeleo.

“Tumekuwa tunatishiwa kwanini mnaongea kwenye vyombo vya habari kila siku, watu wengi wamekuwa wanatutishia, tunatumia uhuru wetu, hatutonyamaza kamwe wakati mambo hayako kimya” amesema.

Ameongeza kuwa “hatuwezi kunyamaza Watanzania wakati rasilimali zetu zinaibwa. Haina mahusiano kabisa na Msomera lakini Ngorongoro ina majukumu makuu matatu, fedha zake zilikuwa zigawanywe kwa mambo makuu matatu uhifadhi, maliasili pamoja na wenyeji.”

Viongozi na wakazi wa Tarafa ya Ngorongoro wamekuwa wakilalamikia zoezi la kuhamisha wakazi hao kutoka katika hifadhi hiyo kwenda kijiji cha Msomera wakidai zoezi hilo si la hiari kwa kuwa linaviashiria vingi vya kutumika kwa nguvu ili kuwaondoa ikiwemo kuzorotesha baadhi ya huduma muhimu kwa wakazi hao ambao wameamua kubaki.

Send this to a friend