Wakenya wachukua mikopo ili kununua vyakula kutokana na mfumuko wa bei

0
35

Baadhi ya Wakenya wamelazimika kuchukua mikopo kwa ajili ya kununua chakula baada ya gharama ya maisha kupanda kwa kiasi kikubwa na kupelekea bei ya vyakula kuwa juu.

Kulingana na utafiti wa Benki ya Dunia, asilimia 12 ya kaya nchini Kenya zimeamua kuchukua mikopo ili kununua chakula kutokana na mfumuko wa bei ya chakula huku asilimia 34 ya kaya wakati huo huo zimeripoti kufanya manunuzi kupitia mikopo katika hali ya mfuko huo wa bei.

Benki ya Dunia imeonya utegemezi wa mikopo kwa kaya kuwa huenda ukachochea madeni huku Wakenya wengi wakiwa hawajui gharama za kukopa.

“Kaya zinaendelea kutegemea kukopa, hali ambayo imeendelea tangu kuanza kwa janga hili, haswa kupitia ukopaji wa muda mfupi. Mwenendo huo unaibua wasiwasi wa kuongezeka kwa madeni, hasa ikizingatiwa kwamba nusu ya Wakenya hawajui gharama halisi ya kukopa,” imesomeka ripoti hiyo.

Rais Samia atangaza kuifumua na kuisuka upya Serikali

Kulingana na utafiti huo, asilimia 60 ya kaya ziliripoti kutegemea mkopo kununua chakula katika siku 30 zilizopita.

Mfumuko wa bei wa vyakula uliongezeka kwa asilimia 15.8 mwezi Oktoba huku mfumuko wa bei ukiwa juu zaidi ya asilimia 9.6 katika mwezi huo kabla ya kupungua kidogo hadi asilimia 9.5 mwezi Novemba.

Send this to a friend