Wakenya wapika na kuuza chang’aa Uarabuni

0
12

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Alfred Mutua amesema kuna baadhi ya raia wa nchi hiyo waishio ughaibuni wanaojihusisha na utengenezaji wa pombe haramu katika nchi za Kiarabu ambapo ni kinyume na sheria.

Ameyasema hayo katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Citizen TV ambapo amedai Wakenya hao wanaofanya shughuli hizo wanahujumu jitihada za Serikali katika kushughulikia masuala ya ustawi wa raia wake nje ya nchi.

“Inasikitisha sana kuna Wakenya ughaibuni wanatengeneza pombe za kienyeji, chang’aa na kuuza kwa Waafrika wengine kinyume na sheria za nchi za Kiislamu,” amesema.

Asilimia 24 ya Watanzania hawajui kusona na kuandika

Aidha, akijibu malalamiko kuhusu baadhi ya Wakenya wanaofanya kazi Saudi Arabia kupitia unyanyasaji mwingi, amesema Serikali inafanya kila iwezalo kuboresha ustawi wa Wakenya katika nchi hiyo, na kwamba aliona hali si mbaya kama inavyosikika wakati alipoitembelea nchi hiyo.

Send this to a friend