Wakenya washindwa kula milo mitatu kwa siku

0
19

Wananchi Kenya wameendelea kutoa malalamiko yao kupitia mitandao ya kijamii kuhusiana na kupanda kwa bei mbalimbali za bidhaa na kufanya iwe vigumu kwao kumudu milo mitatu kwa siku.

Baadhi ya wananchi wamekuwa wakichapisha stakabadhi zao baada ya kununua vyakula, huku wakitumia ‘#lowerfoodprices’ na kuikosoa Serikali kwa kushindwa kuzuia kupanda kwa bei ya bidhaa za kila siku, jambo linalodaiwa kuwa limechangia Maisha kuwa magumu.

 

“Be za Bidhaa kwakweli zimepanda. Hatuwezi kuvumilia Zaidi. Hapo zamani ukiwa na Bajeti ya ununuzi wa $26 ungeweza kuondoka na sanduku lililojaa bidhaa. Leo kiasi hicho hicho kinakupa vitu vichache tu”. Wamesema

 

Aidha, Shirika la Takwimu Kenya (KNBS) limeripoti kuwa mfumuko w bei ulipanda kwa asilimia 8.89 mwezi Januari, huku kodi za juu na gharama kubwa za uzalishaji zikiwa miongoni mwa sababu zinazotajwa kupelekea bei kuongezeka.

 

Hata hivyo athari za Janga la UVIKO 19 pia limetajwa kuwa sababu za kushuka kwa thamani ya shilingi ya Kenya kwa takribani asilimia 6 tangu Mei 2021, kutokana na sekta ya utalii na mauzo ya nje ya nchi kushuka.

 

Send this to a friend