Wakili feki aliyeshinda kesi zote akamatwa

0
59

Mamlaka nchini Kenya imemkamata wakili feki, Brian Mwenda ambaye amekuwa akijitambulisha kama Wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya.

Chama cha Wanasheria cha Kenya (LSK), tawi la Nairobi Rapid Action Team (RAT) kimemkamata tapeli huyo baada ya kupokea malalamishi kutoka kwa umma kuhusu shughuli zake za ulaghai.

NHIF: Mwanachuo hatopata huduma kama hana namba ya NIDA

Kulingana na LSK, Mwenda si wakili na hana leseni ya kufanya kazi ya sheria nchini humo.

Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti, Mwenda alitoa hoja 26 mbele ya majaji wa Mahakama Kuu, mahakimu na majaji wa Mahakama ya Rufani na kushinda kesi zote 26 kabla ya kukamatwa.

Send this to a friend