Wakili wa serikali akamatwa kwa tuhuma ya rushwa

0
17

TAKUKURU Mkoa wa Manyara inamshikiliwa Mwendesha Mashitaka wa mkoa huo, Mutalemwa Kishenyi kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya TZS milioni 5.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, Holle Joseph Makungu amesema Wakili Kishenyi alikamatwa Aprili 23 mjini Babati usiku akiwa anapokea fedha hizo kutoka kwa watuhumiwa wa makosa ya jinai ili awasaidie.

Amesema watuhumiwa hao walikamatwa katika upekuzi uliofanywa na mamlaka za dola ambapo walikamatwa na risasi 370 na stika bandia zenye thamani ya TZS bilioni 6.

“Uchunguzi zaidi wa tuhuma hizi unaendelea na ukikamilika mtuhumiwa huyu atafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma husika,” amesema Makungu.

Send this to a friend