Wakili: Wabunge 19 wataendelea kuwa wabunge, kesi haijafutwa

0
73

Wakili anayeisimamia kesi ya Wabunge 19 waliovuliwa uanachama na Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Emmanuel Ukasu amesema kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama imetupiliwa mbali na mahakama lakini haijafutwa hivyo wataendelea na majukumu yao kama wabunge.

Wakili Ukasu amesema hayo baada ya maswali mengi juu ya wabunge hao kuendelea kushiriki vikao vya bunge licha ya mahakama kutupilia mbali kesi hiyo Juni 22 mwaka huu.

“Kwa sasa siwezi kusema mengi. Ninajadiliana na wateja wangu kujua hatua inayofuata. Wataendelea na majukumu yao kama wabunge,” amesema Ukasu.

Gazeti la Mwananchi limeripoti maoni ya baadhi ya wanasheria juu ya uhalali wa wabunge hao kushiriki vikao vya bunge. Mmoja wa mawakili hao Harold Sungusia amesema kitendo cha mahakama kutoa hukumu tayari wabunge hao hawatakiwi kuwepo bungeni.

Tanzania kupeleka wanajeshi kudhibiti waasi DR Congo

“Mara ya mwisho Spika alisema kwamba hawezi kufanya lolote kwasababu kesi iko mahakamani, sasa kesi haiko mahakamani, tumsubiri anasemaje tena” amesema Sungusia.

Hata hivyo Wakili Sungusia ameongeza kuwa Spika anatakiwa kufuata Katiba inayomtaka mbunge kuwa mwanachama wa chama cha siasa hivyo hapaswi kuwa na kigugumizi kuwaondoa.

Send this to a friend