Wakulima kuanza kupata pensheni ya uzeeni

0
44

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Usimamizi wa Mfumo wa Stakabadhi Ghalani Tanzania, Asangye Bangu amesema wakulima wanaouza mazao yao kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani wanatarajia kuanza kupata pensheni ya uzeeni.

Akizungumza na vyama vya ushirika vya msingi vya Ligunga, Namatili na Mtetesi wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma amesema, Serikali imedhamiria kuhusisha mfumo wa stakabadhi ghalani na pensheni kwa wakulima ili kumudu kuendesha maisha yao wanapokuwa wazee.

Mwanamke mjamzito abakwa na wanaume wanne

“Nguvu zinapokuwa zimepungua, mashamba bado unayo, hivyo pensheni itawezesha wakulima wazee kuendelea kupata fedha za kuwalipa vibarua watakaokuwa wanawafanyia kazi za kilimo,” amesema.

Aidha, amesema pensheni hiyo itaambatana na mambo mengine muhimu kama bima za afya na mikopo, hivyo kwa sasa Serikali iko katika hatua za awali kuhakikisha kuwa suala hilo linafanikiwa.

Send this to a friend