Wakulima Lindi wakataa kuuza korosho zao

0
52

Wakulima wa korosho katika Kata ya Nachunyu, Halmashauri ya Mtama mkoani Lindi wamekataa kuuza korosho zao (tani 1895.6) kutokana na kutoridhika na bei zilizotolewa na wanunuzi.

Wananchi wametoa uamuzi huo leo wakati wa mnada uliofanyika kwenye ghala la Chama cha Ushirika cha Natam (Natam AMCOS) ambapo bei ya juu iliyotolewa ilikuwa TZS 2,275 na ya chini TZS 2,010, huku wao wakitaka walau TZS 3,000 kwa kilo.

Katika mnada huo jumla ya kampuni 12 zimejitokeza na kampuni 11 ziliomba kununua korosho hizo zilizokuwa kwenye maghala matatu ya Bucco Lindi, Mtama na Nangurukuru.

Wananchi wamesema hawatozuza korosho za kwa bei iliyotolewa kwani kwanza baada ya makato mbalimbali hawatopata faida yoyote wakikubali bei hizo, lakini pia bei ya kununua kilo moja iliyotolewa, haifikii gharama ya uzalishaji ambayo ni TZS 2,300.

Mnada huo umehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho, Brigedia Jenerali (Mstaafu) Aloyce Mwanjile na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho, Francis Alfred ambao kwa pamoja wamewahimiza viongozi wa AMCOS na wakulima kuzingatia ubora wa zao la korosho ili kupata bei nzuri na wasiruhusu watu wachache kuharibu soko kwa kuingiza korosho chafu.

Send this to a friend