Wakulima wadai baadhi ya mawakala wanaficha mbegu za ruzuku

0
48

Wakulima wa mikoa ya Songwe na Mbeya, wamelalamikia kitendo kinachofanywa na  baadhi ya mawakala kuficha mbolea ya ruzuku, hali inayowaletea usumbufu mkubwa.

Wamedai baadhi ya mawakala hao hulangua  mbolea ya kukuzia aina ya UREA na kuwauzia bei ya TZS 90,000 badala ya TZS 70,000 iliyotangazwa na Serikali.

Akizungumza na Mwananchi mmoja wa wakulima hao, John Nzunda amesema ni zaidi ya wiki moja sasa kumekuwa na uhaba wa upatikanaji mbolea, hali iliyosababisha kuzuka kwa walanguzi ambao wanauza mbolea hiyo ya ruzuku aina ya UREA kwa bei ya TZS 90,000 tofauti na ile iliyotangazwa na Serikali ya TZS 70,000.

“Tunahisi kuna ujanja, maana tukienda kwa mawakala wengi hawana mbolea matokeo yake tumekuwa tukiahidiwa na kupewa majibu ya kusubirishwa,” amesema

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend