Wakulima watakiwa kujisajili na kupewa vitambulisho

0
41

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wakulima wote nchini kujisajili na kutambulika katika orodha ya wakulima ili kupata huduma stahiki kwa urahisi.

Ameyasema hayo leo wakati akishiriki katika kilele cha maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima iliyofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

“Niombe wakulima wote mwende mkajisajili, mbele huko tutatoa vitambulisho kwa wakulima. Kitambulisho chako ndicho kitakachokufanya uende kupata huduma kadhaa ikiwa ni mkopo, ruzuku au mambo mengine.” Amesema.

Aidha, amesema kwa wale watakaoshindwa kujisajili na majina yao kukosekana katika orodha, watapata taabu mbeleni pindi watakapotaka kupatiwa huduma.

Hata hivyo, Rais Samia amesema Serikali inazungumza na wadau mbalimbali duniani ili kuunga jitihada za kukuza sekta ya kilimo nchini pamoja na kuutumia mradi wa ‘Feed for future’ ambao umerudishwa nchini kuwanufaisha wakulima pamoja na kujenga miundombinu ya wakulima waliopo nchini.

Send this to a friend