Wakunga na Wauguzi 1,330 wafutiwa matokeo

0
44

Baraza la Ukunga na Uuguzi Tanzania limetangaza kufuta matokeo ya mtihani wa usajili na leseni za wauguzi na wakunga kwa watahiniwa wa Stashahada 1,330 uliofanyika Septemba 07, 2023 baada ya kubaini kuwa kuna kuvuja kwa mitihani.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya imesema mtuhumiwa aliyehusika na uvujaji huo, tayari amebainika na amesimamishwa kazi ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Aidha taarifa imesema watahiniwa watapewa nafasi ya kufanya mtihani mwingine bila malipo yoyote na hawatahitajika kujisajili tena, na mtihani huo utafanyika Februari 16, mwaka huu mkoani Dodoma.

Baraza liliendesha mitihani ya usajili na leseni kwa wauguzi na wakunga 1,434 wa ngazi zote, watahiniwa wa Astashahada wakiwa 44, Stashahada 1,330 na Shahada 60 huku mitihani hiyo ikifanyika katika vituo vitatu ikiwemo mkoani Dar es Salaam (DUCE), Mwanza (Mwanza University) pamoja na Dodoma (St. John University).

Send this to a friend