Walimu waliovuliwa vyeo kisa wimbo wa ‘Honey’ warejeshwa kazini

0
41

Walimu wakuu wawili wa shule za msingi Mlimani na Tunduma TC waliovuliwa vyeo vyao na kusimamishwa kazi kufuatia video iliyosambaa mitandaoni ya wanafunzi wakicheza wimbo wa ‘Honey’ wa msanii Zuchu wamerejeshwa kazini.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Seleman Kateti ameeleza kuwa kutokana na kauli ya Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson aliyoitoa bungeni Novemba 06, mwaka huu akiagiza walimu hao kupewa nafasi ya kusikilizwa, halmashauri hiyo imelazimika kuwarudisha kazini kutokana na taratibu kutokufuatwa.

Dkt. Tulia alitoa wito huo kwa Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda kuwa, “kama walimu hao hawakuwepo shuleni na mamlaka ya nidhamu imechukua hatua kabla ya kufanya uchunguzi, basi walimu hao warejeshwe kwenye nafasi zao.”

EWURA yabadili utaratibu kwa waagizaji mafuta

Wito huo ulikuja baada ya kauli ya Waziri Mkenda ambaye alisema endapo adhabu hiyo haikuwatendea haki ikiwemo walimu hao kutokuwepo shuleni siku ya tukio, basi walimu hao wakate rufaa.

Send this to a friend