Walimu waongoza kwa utoro kwa asilimia 66.5

0
36

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange amesema suala la utoro kwa walimu linaongoza kwa asilimia 66.5 huku akiagiza Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) kufuatilia suala hilo na kuchukua hatua.

Imedaiwa kuwa hivi karibuni utoro ambao umeibuka ni walimu kwenda kujiendeleza kimasomo bila kupata kibali cha mwajiri.

BRELA: Hatujapokea malalamiko kuhusu kampuni ya Kalynda

Naibu Waziri ameyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa kwanza wa Baraza la Walimu nchini uliofanyika hapo jana jijini Dodoma.

“Naomba TSC fuatilieni suala hili la utoro, hatuhitaji kuona walimu wanatoroka badala yake wafanye kazi,” amesema.

Amesema Serikali inawajali walimu na kuwataka kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidiI kama walivyoagizwa na Serikali.

Send this to a friend