Walimu waonywa kukesha kwenye vilabu vya pombe

0
46

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema amekemea tabia ya baadhi ya walimu kukesha baa na kwenye vilabu vya pombe za kienyeji kila siku na kuwataka kurudisha hadhi ya walimu iliyokuwepo miaka ya nyuma nchini.

Akizungumza mkoani humo wakati wa uzinduzi wa vitabu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini, Mjema amesisitiza kuwa hadhi ya walimu ambayo ilikuwepo miaka ya nyuma inapaswa kurejeshwa.

Wakamatwa kwa kulaghai na kuwaibia wanawake kwa kutumia madawa

“Zamani ninakumbuka akipita mwalimu mtaani anaheshimika kweli, utasikia yule mwalimu fulani, hata akizungumza jambo kwenye mkutano linazingatiwa, lakini siku hizi heshima hiyo haipo tena, walimu wanalewa tu kwenye baa, wengine wanavaa nguo zisizo na staha yaani vurugu tupu,” amesema Mjema.

Aidha, Mjema amekemea pia tabia ya baadhi ya viongozi na wazazi kuwadhalilisha walimu mbele ya wanafunzi, na kuagiza kuwa mwalimu anapofanya kosa aitwe pembeni na kuonywa, na siyo kudhalilishwa na kushusha heshima yake.

Send this to a friend