Walinzi watatu wauawa wakiwa lindo

0
42

Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni walinzi wa kampuni binafisi za ulinzi katika mtaa wa Shilabela Kata ya Buhalala wilaya ya Geita mkoani humo wameuwawa na mtu ambae hajatambulika wakiwa wanatekeleza majuku yao ya ulinzi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa njia ya simu, Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Geita, Ally Kitumbu amesema aliyefanya mauaji hayo ni mtu mmoja, alipofika eneo la tukio alitumia vipande vya ubao kutekeleza mauaji hayo.

Benki Kuu ya Argentina yapendekeza kuweka sura ya Messi kwenye noti ya 1000

Amesema mpaka sasa jeshi la polisi linaendelea na msako mkali kwa lengo la kuhakikisha wanamkamata mtu huyo aliyehusika na mauaji hayo.

Mkuu wa wilaya Geita, Wilson Shimo amekemea mauaji hayo na kuliagiza jeshi la polisi kuhakikisha uchunguzi unafanyika haraka ili mtu aliyefanya mauaji hayo akamatwe haraka kwa lengo kuchukuliwa hatua za kisheria.

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Shilabela wamesema matukio ya kuuawa kwa walinzi yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara na kuiomba serikali kuhakikisha wanakomesha mauaji hayo.

Send this to a friend