Waliofariki ajali ya ndege ya Precision Air wafikia 19

0
62

 

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema mpaka sasa idadi ya waliofariki katika ajali ya Ndege ya Precision Air kwenye Ziwa Victori mkoani Kagera imefikia 19.

 

Waziri mkuu amesema hayo akiwa katika eneo la ajali baada ya kuwasili mchana wa leo na kuongeza kuwa kwa sasa zoezi linaloendelea ni utambuzi wa watu waliopoteza maisha na kufanya utaratibu wa kuwapata ndugu zao.

 

Aidha, amesema kulingana na idadi iliyotolewa ya watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Bukoba, anaamini kuwa hakuna mwili uliobaki ndani ya ndege.

 

Naye Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila wakati akitoa amesema ukijumuisha idadi ya majeruhi 26 na vifo 19 inakuwa jumla ya idadi 45 na si 43 kama ilivyotajwa mwanzoni hivyo wanaendelea kujiridhisha kujua kama idadi halisi ya abiria ilikuwa 43 au zaidi.

 

“Ukijumlisha majeruhi 26 na na vifo 19 inakuwa 45 na sio 43 tuliyoambiwa mwanzoni […] Tunaendelea kujiridhisha kujua kama idadi halisi ya watu ilikuwa 43 au zaidi. Inawezekana katika maokozi watu wawili ambao hawakuwa wasafiri wamepoteza maisha,” amesema.

Send this to a friend