Waliohamia CCM waangukia pua kura za maoni

0
51

Waliokuwa wanachama wa vyama vya upinzani nchini Tanzania ambao kwa nyakati tofauti walihama vyama vyao na kujiunga Chama cha Mapinduzi (CCM) wameshindwa kutamba kwenye kura za maoni.

Wanasiasa hao ambao wengi walikuwa wabunge wakati wakihama walichukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kugombea ubunge lakini wamefanya vibaya katika hatua za awali.

Wanasiasa hao ni pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye amepata kura 2 katika Jimbo la Kawe, Joshua Nassari aliyepata kura 26 katika Jimbo la Arumeru Mashariki na Abdallah Mtolea ambaye amepata kura 22 katika Jimbo la Temeke.

Wengine ni Maulid Mtulia aliyepata kura 11 katika Jimbo la Kinondoni, David Silinde aliyepata kura 118 katika Jimbo la Tunduma, Peter Lijualikali amepata kura 5 katika Jimbo la Kilombero na Patrobas Katambi aliyepata kura 12 katika Jimbo la Shinyanga Mjini.

Mchakato wa kura za maoni ndani ya chama hicho unafikia tamati leo ambapo majimbo yote yanatakiwa yawe yamekamisha kupata mshindi tayari kuruhusu hatua nyingine za mchakato.

Send this to a friend