Walioiba milioni 47 na kuficha benki wakamatwa

0
39

Jeshi la Polisi mkoani Manyara linawashikilia Juma Athumani (23) na Mariam Mbega (26) kwa tuhuma za kuvunja nyumba na kuiba TZS milioni 47 za mfanyabiashara Laurent Elias ambaye ni mkazi wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Manyara, ACP Goerge Katabazi amesema tukio hilo limetokea Juni 6 mwaka huu katika Mji Mdogo wa Mirerani ambapo baada ya uhalifu wa kuiba fedha hizo watuhumiwa hao walizificha kwa kuziweka kwenye akaunti zao za benki ili wasibainike.

Dkt.Tulia ayaonya Nipashe na The Guardian upotoshaji suala la Bandari

Kamanda Katabazi amesema Jeshi la Polisi limezuia fedha hizo zisitoke benki ili taratibu za kisheria zifuatwe, na kwamba watuhumiwa hao wanashikiliwa na Polisi kwa upelelezi zaidi.

Send this to a friend