Waliojifanya maafisa TRA Arusha wakamatwa

0
28

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha  linawashikilia watuhumiwa watano kwa tuhuma za kujifanya maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kutapeli wananchi katika maeneo mbalimbali mkoani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Fredy Malaki (34) mkazi wa Karakata, Francis Mwita (42, Fidelis Joseph (27) , Selina Fortunatus (43) wote kutoka Jijini Dar es salaam na Fereji Hamadi (40) mkazi wa Tabora.

ACP Masejo amebainisha kuwa bado Jeshi hilo linaendelea kuwahoji watuhumiwa hao na pindi upelelezi utakapo kamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtka kwa hatua zaidi za kisheria.

Sambamba na hilo ACP Masejo ametoa wito kwa wananchi kujiridhisha na watu wanaofika maeneo yao ya biashara na kujitambulisha kuwa ni maafisa wa TRA na kuwaomba wananchi kutoa taarifa za baadhi ya watu hao wachache wanaofanya matukio ya uhalifu hususani ya utapeli katika Mkoa huo ili hatua za kisheria ziendelee kuchukuliwa dhidi yao.