Waliokamatwa Loliondo washtakiwa kwa mauaji ya askari polisi

0
48

Baada ya kuripotiwa kwa taarifa ya kuuawa askari polisi Garlus Mwita (36) kwa kupigwa mshale, katika zoezi la uwekaji mpaka Loliondo, watu 20 akiwemo Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ngorongoro mkoani Arusha, Ndirango Senge Laizer wemefikishwa mahakama ya Hakimu  Mkazi Arusha kwa shtaka la mauaji kwa kukusudia.

Mbali na Mwenyekiti huyo, wengine waliofikishwa mahakamani ni pamoja na madiwani wa CCM kutoka kwenye baadhi ya Kata za Loliondo.

Taarifa zinasema kuwa washtakiwa hao walipofikishwa mahakamani hapo walisomewa mashtaka hayo na kisha kupelekwa gereza kuu la Kisongo lililopo jijini Arusha kutokana na tuhuma zinazowakabili kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, bado haijafahamika kama washtakiwa hao waliofikishwa mahakamani wanakabiliwa na mashtaka mengine au la.

Garlus aliuawa Juni 10 mwaka huu huko Loliondo kwa kuchomwa mkuki na watu wasiojulikana wakati yeye na askari wenzake walipokuwa wakiimarisha usalama kwenye kazi ya uwekaji wa alama za mipaka.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend