Waliokosa GPA ya 4.4 wazuiwa kuhudhuria mahafali

0
51

Chuo Kikuu cha Ibadan nchini Nigeria kimewazuia wahitimu waliopata ufaulu (GPA) chini ya daraja la kwanza kuhudhuria sherehe za mahafali ya kuitimu elimu ya juu.

Chuo hicho kikongwe nchini Nigeria kimewataka wale wote ambao hawajapa ufaulu wa daraja la kwanza kufuatilia mahafali hayo kupitia mtandao.

Aidha, wazazi na wageni wengine wamezuiwa kuhudhuria mahafali ya watoto wao, na pia hakutakuwa na burudani yoyote au mkusanyiko wa kijamii wakati wa mahafali hayo.

Chuo hicho kimesema kuwa uamuzi huo wa kuwaacha baadhi ya wanafunzi unalenga kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona.

Mahafali ya chuo hicho yanatarajiwa kufanyika wiki mbili zijazo.

Send this to a friend