Waliomwagiana maji ya dripu kwenye birthday wasimamishwa kazi

0
18

Uongozi wa Hospitali ya Sakamu umewasimamisha kazi watumishi wa hospitali hiyo kupisha uchunguzi baada ya video iliyosambaa mitandaoni ikiwaonesha wakimmwagia mwenzao maji ya dripu kama njia ya kumpongeza kwenye siku yake ya kuzaliwa, Desemba 1.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Sakamu, Salvatory Musimu amesema wahusika hao ni watumishi wa hospitali binafsi ya Sakamu iliyopo Geita Mjini mkoa wa Geita na siyo kituo cha Afya Nyankumbu kama ilivyoelezwa.

Aidha, uongozi wa hospitali hiyo umeomba radhi kwa kile kilichotokea na kuahidi kusimamia taratibu na miongozo ya afya kwa hatua zaidi dhidi ya wahusika.

Send this to a friend