Walioondolewa kazini kwa vyeti feki kupewa michango yao ya hifadhi ya jamii

0
60

Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia watumishi walioondolewa kazini kwa sababu za kughushi vyeti kurudishiwa michango yao waliochangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Ameyasema hayo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo ametaja mfuko wa PSSSF ni asilimia 5 na kwa NSSF ni asilimia 10 ya mshahara wa mhusika, na kwamba haitohusisha malipo mengine yoyote ya ziada.

Ameongeza kuwa marejesho hayo kwa watumishi yataanza kufanyika Novemba 1, 2022, na ili kuwezesha kupata malipo hayo mtumishi atahitajika kwenda kwa aliyekuwa mwajiri wake akiwa na baadhi ya nyaraka ambazo ni picha 2, ‘passportsize’ nakala za kibenki kwa akaunti iliyo hai, kitambulisho cha uraia, cha mpiga kura au leseni ya udereva.

Aidha, amesisitiza kuwa waajiri ndio watakaowajibiika kuwasilisha nyaraka hizo kwenye mifuko ili kuwezesha kufanyika kwa malipo hayo.

Send this to a friend