Waliopandikizwa uume waweza kujamiiana tena

0
48

Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika amesema huduma ya kupandikiza uume kwa wagonjwa wawili waliokuwa na changamoto ya nguvu za kiume imeleta matokeo chanya.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma amesema zoezi hilo lilifanyika kwa mara ya kwanza Juni mwaka huu baada ya kubaini changamoto kubwa iliyopo kwa baadhi ya wanaume kukosa nguvu hizo.

“Tulianza kutoa hii huduma mwezi wa sita kwa kuwahudumia wanaume wawili tu, lakini kwa habari njema kutoka kwao, mambo ni mazuri sana kwa sababu tuliwapa masharti wakae wiki sita ndipo waweze kujaribu mitambo, mitambo imefanya kazi vizuri. Hizo ni taarifa kutoka kwao wenyewe kwa sababu tunaendelea kuwafuatilia na matokeo ni mazuri sana,” amesema.

Ameongeza kuwa hospitali hiyo iko katika harakati za kuongeza wigo wa utoaji wa huduma hiyo ili wananchi wengi waweze kupatiwa huduma kwa urahisi zaidi na kwamba watashirikiana na hospitali nyingine ili kujua namna ya kupata vipandikizi hivyo pamoja na kuwapa mafunzo ili kuwafikia wananchi wengi.

Aidha, Dkt. Chandika amebainisha kuwa gharama za huduma hiyo ni shilingi mlioni 6 hadi milioni 10.

Send this to a friend